Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar Imesaini Hati ya Makubaliano ya Mfumo wa Taarifa za Usimamizi na Usajili wa Ardhi Zanzibar iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ndg Khadija Khamis Khamis Rajab na Meneja Mkuu wa Taasisi ya Kitaifa ya Kijiografia na Misitu (IGN FI) ya Ufaransa Christophe Dekeyne
Hafla ya utiaji saini imefanyika Agosti 7/2024, katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat AL-Bahr Mazizini Zanzibar
Naibu Waziri Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar.Mhe. Salha Muhammed Mwinjuma amesema Wizara itahakikisha itawalipa fidia wananchi wote ambao vipando vyao viliathiriwa kwa ajili ya kupisha ujenzi wa Nyumba za gharama nafuu ambapo zinatarajiwa kujengwa katika eneo la Chumbuni.
Mhe. Salha ameyasema hayo wakati wa kikao cha pamoja baina ya Uongozi wa Wizara, Mkoa, Jimbo na wananchi huko Chumbuni Mkoa wa Mjini Magharibi kuwa Serikali ipo tayari kwa ujenzi huo na inaendelea na zoezi la uthamini katika eneo hilo pia hakuna mwananchi atakaedhulumiwa wala kukosa haki zake juu ya fidia hiyo kulingana na miongozo
Wafanyabiashara wa mabanda ya papa katika eneo la Malindi wamempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kuwatatulia kilio chao cha muda mrefu cha kushushiwa bei ya kodi kwa milango wanayoitumia inayomilikiwa na Shirika la Nyumba Zanzibar.
Wafanyabiashara wa mabanda ya papa katika eneo la Malindi wamempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kuwatatulia kilio chao cha muda mrefu cha kushushiwa bei ya kodi kwa milango wanayoitumia inayomilikiwa na Shirika la Nyumba Zanzibar.Wafanyabiasha hao wametoa pongezi hizo wakati Naibu Waziri wa wizara ya Ardhi