Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Kamisheni ya Ardhi

Kamisheni ya Ardhi ni chombo cha Serikali kilichoanzishwa kupitia Sheria Namba 6 ya mwaka 2015 (THE COMMISSION OF LANDS ACT NO 6 OF 2015) . Lengo la kuanzishwa Kamisheni ya Ardhi ni kusimamia maswala ya ardhi katika kujenga uimara wa uongozi na rasilimali ya ardhi kwa ajili ya matumizi bora na maendeleo ya Taifa. Ili kutimiza azma hiyo imeonekana ni vyema kuanzishwa chombo ambacho kitakuwa na uwezo wa kusimamia mambo yanayohusu ardhi kwa ujumla wake. Chombo hiki kinaongozwa na Katibu Mtendaji.

Sababu za kuanzishwa Kamisheni ya Ardhi

Kuna sababu kadhaa zilizopelekea kuanzishwa Kamisheni ya Ardhi miongoni mwa sababu hizo ni hizi zifuatazo:-

i) Kuwa na chombo kimoja kinachounganisha Taasisi zote zinazosimamia Ardhi

Kamisheni ya Ardhi imeundwa ili iwe chombo kinachounganisha Idara zote za ardhi katika mwamvuli na Chini ya uongozi mmoja.Hapo awali kabla ya kuanzishwa chombo hiki utawala wa ardhi na usimamizi ulikuwa umegawika kiidara ambapo kila Idara ilikuwa inafanya kazi zake wenyewe bila ya kuwepo chombo ambacho kinaunganisha Idara zote za ardhi.

ii)Kurahisisha utoaji wa huduma katika muhimili mmoja.

Kuwa na taasisi tofauti ambazo zinasimamia masuala ya ardhi kulipelekea kuweko na urasimu katika utolewaji wa huduma katika sekta ya ardhi. Hivyo Serikali iliamua kuunda taasisi ambayo itaziunganisha Taasisi zote za ardhi na hivyo kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi.

iii)  Kusimamia Sheria na Sera ya Ardhi.

Kutokuwepo kwa chombo kimoja kinachosimamia utekelezaji wa Sheria na Sera ya Ardhi kulipelekea kurejesha nyuma usimamizi na utekelezaji wa Sheria za Ardhi. Hivyo Kamisheni ya Ardhi iliundwa ili iwe na Mamlaka kamili ya kusimamia sheria zoteza Ardhi pamoja na Sera ya Ardhi.

MAJUKUMU YA KAMISHENI YA ARDHI

Kamisheni ya Ardhi ni chombo kikuu katika utendaji wa mambo yote yanayohusiana na Uongozi na Usimamizi wa Ardhi, kwa Mujibu wa Sheria Nam. 6 ya mwaka 2015, sura ya Il kifungu Nam. 4, imepangiwa majukumu makuu yafuatayo:-

  1.   Kupendekeza na kushauri utekelezaji wa sera ya ardhi.
  2.     Kuishauri Serikali juu ya mpango mahsusi kwaajili ya usajili wa Ardhi ya Zanzibar.
  3.     Kusimamia usajili wa haki na masłahi yote katika ardhi.
  4.     Kudhibiti uhaulishaji wa haki au masłahi yaardhi iliyokuwa haijasajiliwa.
  5.    Kuratibu Mpango wa Matumizi ya Ardhi kitaifa kwaajili ya nchi nzima.
  6.      Kuainisha viwango (standards) na vigezo (noms) vya utawala wa Ardhi (land administration).
  7.    Kupendekeza mipango ya kuhakikisha sera za Serekali, ikiwemo maendeleo ya ardhi, inafanya kwa usahihi zaidi ardhini.
  8.      Kuyafanyia kazi masuala yote ya utendaji na maelekezo ya Waziri yanayohusiana na uongozi pamoja na usimamizi wa Ardhi.
  9.   Kuyafanyia kazi majukumu na matakwa yalioelezwa katika sheria ya haki ya matumizi ya ardhi (land tenure Act) pamoja na marekebisho yake.
  10.    Kufanya utafiti katika masuala yanayohusiana na ardhi.
  11.    Kushauri na kusimamia miradi ya kimaendeleo.
  12.    Kuanzisha chombo kwa ajili ya kuongoza shughuli zote zinazohusiana na utawala wa ardhi
  13.    Kuanzisha na kuhakikisha kunakuepo na uhusiano wa taasisi nyengine za kitaifa na za kimataifa zinaohusiana na mambo ya ardhi
  14.    Kupitia sheria za ardhi zilizopo na panapohitaji marekebisho hayo yafanyike.
  15.    Kuandaa na kushajihisha mpango mkakati wa elimu kwa ujumla katika matumizi ya ardhi na usimamizi wa ardhi kwa ajili ya kuleta uwelewa kwa umma juu ya uhifadhi wa ardhi na kuiendeleza.
  16.   Kuratibu shughuli za taasisi zote zinazohusiana na Ardhi na kuwa ni chombo au chanzo cha mawasiliano kati ya taasisi hizi na Serikali.
  17.   Kuratibu shughuli zote za Upimaji na Ramani zote za Zanzibar.
  18.   Kuendeleza na kuhifadhi mfumo sahihi wa taarifa za usimamizi wa Ardhi.
KWA MAWASILIANO ZAIDI FIKA OFISINI KWAO FORODHANI AU WASILIANA NAO:

142 BARABARA
YA KANSA KATOLIKI FORODHALI,

71124 MJINI MAGHARIBI, ZANZIBAR

S.L.P 811

Namba za simu :- 0774 – 776619

Barua pepe: info@kamisheniardhi.go.tz 

Tovuti :  www.kamisheniardhi.go.tz