Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Utumishi na Uendeshaji

IDARA YA UTUMISHI NA UENDESHAJI

UONGOZI

Mkurugenzi katika idara ya Utumishi na Uendeshaji ni ndugu Khamisuu Hamid Mohammed

UTANGULIZI

Idara ya Uendeshaji na Utumishi ndio kiungo muhimu cha Taasisi zote zilizomo ndani ya Wizara. Idara hii ina dhamana ya kusimamia masuala yote ya  kiutawala na kiutumishi katika Wizara na ina jukumu la kusimamia rasilimali watu. Idara hii ina wajibu wa kuwaendeleza watendaji kielimu ili kuhakikisha ufanisi unapatikana katika uendelezaji wa kazi za kila siku za Wizara. Idara hii inasimamiwa na Mkurugenzi ambae huteuliwa na Mheshimiwa Rais.

KAZI KUU

 • Kutoa huduma za uongozi wa Rasilimali Watu na Utawala kwa wizara husika.
 • Kusimamia majukumu ya vitengo vilivyo chini ya Idara.
 • Kusimamia masuala ya ajira, mafunzo, kupandishwa vyeo kwa wafanyakazi wa Wizara.
 • Kuhakikisha kuwepo kwa watendaji wa kutosha na wenye sifa na kuweka kumbukumbu za masuala mbalimbali yahusuyo watendaji.
 • Kufanya tathmini ya utendaji wa kila mtumishi wa Wizara na kuandaa ripoti ya hali ya utumishi kila baada ya muda kwa mujibu matakwa ya sheria au maagizo maalum.
 • Kuratibu masuala Mtambuka yakiwemo (Ukimwi, Jinsia, Mabadiliko ya Hali ya nchi, mambo ya idadi ya watu).
 • Kutoa huduma za kitaalamu na huduma za manunuzi na uhifadhi wa vifaa kwa ajili ya Idara nyengine.
 • Kutoa huduma za uhasibu ikiwa ni pamoja na uwekaji wa kumbukumbu za hesabu, mapato na matumizi, ulipaji wa mishahara na matayarisho ya mafao ya uzeeni.
 • Kuandaa na kusimamia mpango kazi wa Idara.
 • Kuandaa na kusimamia bajeti ya Idara.
 • Kufanya kazi nyenginezo kama zitakavyoelekezwa na Uongozi wa Wizara kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za kazi.

KITENGO CHA UENDESHAJI

(Kitaongozwa na Ofisa Utawala Mkuu).

Majukumu:

 1. Kuweka kumbukumbu za matukio muhimu katika sehemu ya kazi
 2. Kusaidi kusimamia nidhamu ya wafanyakazi.
 3. Kuainisha maatatizo ya wafanyakazi.
 4. Kusimamia matumizi na matunzo ya vifaa vya wizara ikiwemo vyombo vya usafiri, magari, mitambo, samani, vifaa vya kuandikia na vifaa vya mawasiliano.
 5. Kusimamia majengo na mali nyengine zisizohamishika.
 6. Kusimamia shughuli za kiufundi na uendeshaji wa maghala ya Wizara.
 7. Kufanya kazi zote atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.

KITENGO CHA UTUMISHI

(Kitaongozwa na Ofisa Mkuu Utumishi).

Majukumu:

 1. Kutunza kumbukumbu sahihi za watumishi wote kulingana na rnahali alipo.
 2. Kukusanya takwimu na kumbukumbu zote zinazohusu mipango ya watumishi.
 3. Kusaidia kukadiria idadi ya watumishi wanohitaji mafunzo.
 4. Kufanya kazi zote atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.

KITENGO CHA UTUNZAJI KUMBUKUMBU

(Kitaongozwa na Ofisa Kumbukumbu Mkuu)

Majukumu:

 1. Kutafuta kumbukurnbu/nvaraka/rnafaili yanayohitajiwa na wasomaji.
 2. Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa kurnbukumbu/nvaraka.
 3. Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukurnbu/nvaraka katika makundi
  kulingana na somo husika (classification and boxing) kwa ajili ya matumizi ya ofisi.
 4. Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki (file racks/cabinets) katika masjala/vyurnba vya kuhifadhia kumbukumbu.
 5. Kuweka kumbukumbu (barua, nyaraka nk.) katika mafaili.
 6. Kushughulikia maombi ya kumbukumbu /nyaraka kutoka Taasisi za Serikali.
 7. Kufanya kazi nyengine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.