Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Mipango Sera na Utafiti

IDARA YA MIPANGO, SERA NA UTAFITI

UONGOZI

Mkurugenzi katika idara ya mipango sera na utafiti ni ndugu ILIYASA PAKACHA HAJI

UTANGULIZI

Idara ya Mipango, Sera na Utafiti ndio muhimili mkuu wa kuziunganisha taasisi zote zilizomo ndani ya Wizara. Idara hii inajukumu kubwa la kusimamia na kuratibu mipango yote ya Wizara ikiwemo utayarishaji wa Sera, Sheria, Bajeti pamoja na Miradi ya Maendeleo.  

KAZI KUU

  • Kuratibu na kusimamia mipango inayoendeshwa na Wizara.
  • Kuunda na kuratibu sera na sheria.
  • Kupanga, kubuni na kusimamia miradi na programu.
    Kuandaa mipango ya kila mwaka, kuweka mikakati na bajeti ya kila mwaka ya Wizara.
  • Kuratibu shughuli za utafiti wa Wizara na kuandaa ripoti ya utafiti.
  • Kukagua, kuimarisha na kuratibu mipango na programu za maendeleo ya wizara.
  • Kupitia na kutathmini utekelezaji wa sera, mipango, mipango na mradi ya wizara.

Kuratibu, kufuatilia na kusimamia miradi na programu inayofadhiliwa

KITENGO CHA UFUATILIAJI NA TAHMINI (Kitaongozwa na Ofisa Uchumi Mkuu)    

   Majukumu:

  1. Kuandaa viashiria vya taarifa ya ufuatiliaji kwa kuzingatia mahitaji ya Mpango Mkuu wa Ufuatiliaj wa MKUZA.
  2. Kutayarisha mfumo wa muundo wa ukusanyaji wa taarifa na ripoti za utekelezaji
  3. Kuandaa na kushiriki ziara za ufuatiliaji na tathmini zinazofanyika na kuhakikisha zinafuata mifumo iliyokubalika katika ukusanyaji wa taarifa ili ziweze kusaidia katika kutoa maamuzi ya uongozi.
  4. Kuanzisha mfumo bora wa kujifunza kwa kuweka mfumo mzuri wa taarifa, kubadilishana mawazo na kukusanya matokeo ya tathmini na ufuatiliaji.
  5. Kufuatilia utekelezaji wa mpango wa mwaka na Mpango Mkakati wa muda wa kati wa Wizara
  6. Kutayarisha ripoti za utekelezaji wa majukumu ya Wizara Wiki, mwezi, miezi mitatu, nusu mwaka na mwaka.
  7. Kukusanya taarifa za uchambuzi wa takwimu/taarifa zinazohitajika katika kutayarisha Sera, Mipango pamoja na mapendekezo ya bajeti.
  8. Kushiriki katika kutayarisha mipango, programu na shughuli za bajeti za Wizara ikiwemo kutayarisha malengo halisi ya utekelezaji na viashiria.
  9. Kutoa ushauri wa kitaalamu ikiwemo kuanzisha mfumo wa ufuatiliaji na kutathmini ndani ya Wizara
  10. Kushirkiana na kitengo cha ufuatiliaji na Tathmini cha MKUZA katika kutoa na kupokea taarifa za uhakika katika kutayarisha ripoti ya mwaka ya MKUZA, ripoti ya MDGs na Mpango kazi Istanbul.
  11. Kufanya majukumu mengineyo yanayohitajika na Idara ili kufikia Malengo ya Wizara.

KITENGO CHA MAENDELEO YA SERA (Kitaongozwa na Ofisa Uchumi Mkuu)    

Majukumu:

  1. Kutayarisha Sera zinazohitajika na kushauri kwa uongozi.
  2. Kuzichambua Sera ziliopo za Wizara kwa ajili ya kuweka mazingira bora ya Utekelezaji
  3. Kufanya uchambuzi wa masuala ya Kiuchumi, Kijamii na kiutawala na kuishauri Wizara kutayarisha Sera zinazohitajika.
  4. Kuwasiliana na kufanya kazi pamoja na Tume ya Mipango wakati wa kutayarisha na kutekeleza Sera mpya ili kuhakikisha kuwa zinakwenda sambamba na utekelezaji wa Mipango ya Kitaifa ikiwemo MKUZA II, Dira ya 2020 pamoja na Mipango Mikakati ya Mawizara, maidara na Taasisi za serikali.

KITENGO CHA UTAFITI (Kitaongozwa na Ofisa Uchumi Mkuu)

Majukumu:

 1 Kufanya tafiti na uchambuzi za utekelezaji wa Mipango, Miradi na Programu mbali mbali inayotekelezwa na Wizara na kutayarisha maelezo   ya kisekta.

  2 Kufanya uchunguzi juu ya namna ya utoaji wa huduma na kukusanya mawazo/maoni kwa wadau juu ya huduma zinazotolewa na mawizara.

 3 Kushirikiana na Vyuo vya Elimu ya juu katika kufanya tafiti na uchunguzi unaohusiana na majukumu ya Wizara na kusaidia kazi za Idara ya Uchumi na maendeleo katika kutekeleza majukumu yao.

MIPANGO YA KISEKTA NA MAENDELEO (Kitaongozwa na ofisa Uchumi Mkuu).

Majukumu:

1.Kukusanya taarifa na kutayarisha Mpango wa kazi wa mwaka pamoja na Mpango mkakati wa muda wa kati wa Wizara

2. Kuwasiliana na kufanya kazi pamoja na Tume ya Mipango wakati wa kutayarisha mipango mipya ili kuhakikisha kuwa zinakwenda sambamba na utekelezaji wa Mipango ya Kitaifa ikiwemo MKUZA II, Dira ya 2020 pamoja na Mikakati ya Mawizara, Maidara na Taasisi za Serikali

    3. Kuratibu utayarishaji na utekelezaji wa bajeti ya Wizara

    4 .Kukusanya taarifa za miradi/Programu na Mipango kazi ya Wizara.

    5. Kushirikiana na Ofisi ya Raisi, Fedha Uchumi na Mipango ya maendeleo katika kutayarisha Mpango Mkakati na Bajeti ya Wizara.

    6. Kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya kutekeleza Mpango Mkakati wa Wizara na kutayarisha bajeti ya Wizara

    7.Kukusanya taarifa za mapitio ya utekelezaji za kpindi cha muda wa kati na mwaka za Wizara.

    8 .Kukusanya taarifa za takwimu zinazohitajika katika kubainisha vipaumbele vya uchumi, ustawi na maendeleo ya jamii.

    9.Kuratibu Utekelezaji wa maamuzi ya Serikali juu ya masuala ya mipango na uongozi wa masuala ya kiuchumi ya Wizara.

    10.Kushirikisha sekta binafsi katika kazi mbalimbali za maendeleo ya Wizara

    11.Kufanya utafiti juu ya masuala mbali mblai yatokanayo na utekelezaji wa sera za uchumi.

    12.Kufanya utafiti na kubainisha fursa ziliopo sekta husika.

    13. Kukusanya taarifa na takwimu zinazohitajika katika kubainisha vipaumbele vya ustawi na Maendeleo ya jamii.

    14.Kuchambua na kutafsiri (Interpret) takwimu na taarifa mbali mbali za kiuchumi.

    15.Kufanya kazi nyengine zinazolingana na majukumu yake kama atakayopangiwa na mkuu wake.