Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Wafanyabiashara wa mabanda ya papa katika eneo la Malindi wamempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kuwatatulia kilio chao cha muda mrefu cha kushushiwa bei ya kodi kwa milango wanayoitumia inayomilikiwa na Shirika la Nyumba Zanzibar.

Wafanyabiasha hao wametoa pongezi hizo wakati Naibu Waziri wa wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi alipofika katika maeneo hayo kwa ajili ya kuskiliza na kutatua changamoto walizokuwa wakizilalamikia.
Akizungumza mara baada ya kuskiliza changamoto za wafanyabiashara hao Naibu Waziri Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Mhe. Salha Mohamed Mwijuma amesema kufika kwa viongozi wa wizara katika maeneo hayo ni kutekeleza agizo la Mhe. Rais kutokana na imani alionayo kwa wananchi wake.
Mhe. Naibu Waziri amesema Wizara imefikia uamuzi wa kuwapunguzia bei wafanyabiashara kwa waliokuwa wakilipa laki nne na nusu (450,000) sasa wameruhusiwa kulipa lakini tatu (300,000) na kwa wale waliokuwa wakilipa laki tatu na kumi (310,000) sasa wameruhusiwa kulipa laki mbili na nusu (250,000).