Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Bodi ya Usajili Wakandarasi-Zanzibar

Bodi ya Usąjili wa Wakandarasi ilianzishwa kwa sheria nam. 6 ya mwaka 2008 kwa lengo la kusimamia wakandarasi wote na kuhakikisha wanąienga kwa kufuata viwango, pamoja na kanuni na taratibu zote zikiwemo za usalama katika maeneo ya ujenzi zinafuatwa. Bodi hii ina Mwenyekiti ambaye huteuliwa na Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na inakuwa na wajumbe sita wanaoteuliwa na Mhe. Waziri husika na masuala ya ujenzi. Baada ya kupitishwa sheria hiyo, mwaka 2011 Bodi ilianza kufanya kazi zake na kutafuta watendaji wa kuanzimwa katika taasisi mbali mbali za ujenzi za Serikali nchini.

MAJUKUMU:

  1. Bodi ya Usąjili wa Wakandarasi Zanzibar ni chombo kinachojitegemea chenye jukumu la msingi la kusajili na kuwasimamia wakandarasi wa ujenzi na kuwaendeleza kitaaluma pamoja na kusajili miradi yao kama sheria inavyoelekeza.
  2. Kuchukuwa hatua za kinidhamu dhidi ya wakandarasi waliosajiliwa wanaokiuka masharti ya usajili, sheria na kanuni.
  3. Kuandaa na kupeleka Ripoti kila mwaka kwa Mhe, Waziri juu ya utekelezaji wa Majukumu, wajibu na uwezo wa Bodi chini ya sheria hii.
  4. Kutekeleza majukumu mengine yoyote ambayo ni kwa maslahi ya umma na ambayo Waziri husika ataelekeza.

KWA MAWASILIANO ZAIDI FIKA OFISINI KWAO AMANI VIWANDA VIDOGO VIDOGO AU WASLIANA NAO:

P.O.BOX 693 ZANZIBAR, TANZANIA.

Tel: +255 775 064 534

EMAIL: znzcrb@zanlik.com