October 2024
Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Mhe Rahma Kassim Ali akizungumza katika Mkutano wa pamoja kati ya Taasisi inayoshughulikia Masuala ya Nyumba na Fedha Afrika(AUHF)kwa kushirikiana na Jumuiya ya Kimataifa inayoshughulika na Mikopo ya Nyumba(ISMMA) Hafla iliyofanyika katika Hotel ya Melia Kiwengwa Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Mkutano huo Umefunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi ambapo Lengo kuu ni Kuwakutanisha Wanachama Pamoja na Wadau mbalimbali kuzungumzia kuhusiana na Uimarishaji na Uboreshaji wa Makaazi bora na nafuu Afrika na Duniani Kote
Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi imeshauriwa kuhakikisha inaendelea na hatua ya utoaji wa Elimu kwa wananchi kuhusiana utaratibu wa Tozo za Ardhi.
Akizungumza katika kikao Maalumu cha Kamati ya Kanuni na Sheria ndogo ndogo ya Baraza la Wawakilishi kilichowashirikisha Wajumbe wa Kamati hiyo watendaji wakuu wa Taasisi pamoja na Wadau wa Kanuni huko katika Ukumbi wa Wizara ya Ardhi Ofisi kuu Pemba Mwenyekiti wa Kamati Mhe.Mihayo Juma Nunga amesema hatua hiyo itasaidia kuondoa Migongano katika Jamii. Wakichangia