Kampuni inayoshughulika na miradi ya kigeografia kutoka nchini ufarasa imetakiwa kuharakisha ripoti ya upembuzi yakinifu ili kwenda sambamba na wakati uliowekwa.
Katibu mkuu wizara ya ardhi na maendeleo ya makaazi dk.mngereza mzee miraji ameyasema hayo huko katika ukumbi wa wizara hiyo maisara katika kikao cha pamoja na watendaji wa kampuni hiyo pamoja na wajumbe kutoka taasisi mbalimbali za serikali.
Alifahamisha kuwa ripoti hiyo ni vyema ikazingatia muda kufanya hivyo kutapelekea kurahisisha utendaji kazi kwa ufanisi zaidi.
Aidha dk.mngereza amewataka wadau pia kutoa mashirikiano
Kwa kutoa taarifa kamili zitakazowezesha kukamilika kwa zoezi hilo.
Kwa upande wao baadhi ya watendaji wa kampuni hiyo wamewaomba wadau kuhakikisha wanazingatia mda katika utoaji wa taarifa kutoka katika taasisi zao hatua itakayosaidia kuimarisha kwa ripoti ya upembuzi yakinifu