Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Dkt Mngereza Mzee Miraji na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (SMT) Ludovick Nduhiye wakikibidhiana hati ya mashikiriano sekta ya Ujenzi baina ya Serikali zote mbili katika ukumbu wa Madinat Albahar Mbweni-Zanzibar

WAZIRI wa Ujenzi  na Uchukuzi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Prof.Makame Mnyaa Mbarawa amezitaka Taasisi za SMT na SMZ zinazosimamia masuala ya ujenzi kuhakikisha wanawajengea uwezo wahandisi pamoja na wataalamu wa masuala ya ujenzi ili kuweza kufanyakazi hizo kiutaalamu zaidi.

Aliyasema hayo wakati alipokua akifunga kikao cha mashirikiano sekta ya Ujenzi baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kilichowashowashirikisha Makatibu Wakuu,Manaibu Makatibu Wakuu,Wahandisi pamoja watendaji wa Taasisi pamoja na watendaji wa Taasisi hizo huko katika ukumbi wa Madinatul-Bahari Mbweni.

Alifahamisha kua nchi ya Tanzania ina fursa nyingi na miradi mbalimbali hivyo ni vyema Taasisi zote mbili kuzitumia fursa hizo kwa kuekeza zaidi katika kuwajengea uwezo wataalamu wetu wa ndani na kuondokana na kuagizia wataalamu kutoka nje ya nchi.

”nizitake taasisi zote mbili kuhakikisha zinatumia fursa tulizonazo katka kuwajengea uwezo wataalamu wetu ili kuondoka na na changamoto ya kuagiza wataalamu hao kutoka nje ya nchi”├ílisisitiza Mhe.Pro.Mbarawa.

Aidha Prof.Mbarawa alisisitiza haja pia kwa Taasisi hizo kuandaa mipango maalum ambayo itaweka mikakati imara na kuchochea ushiriki wa wanawake katika sekta ya ujenzi amabyo imeonekana kuna uhaba wa wataalamu hao kwa upande wa wanawake.

Kwa upande wake Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za Serikali Mhe.Masoud Ali Mohammed alisema kua ni vyema kwa taasisi zote mbili kuyafanyia kazi maelekezo yote kwa lengo la kuleta mabadiliko ya kimaendeleo hasa katika sekta ya ujenzi.

Akizungumzia kuhusiana na kikao  hicho Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Dkt.Mngereza Mzee Miraji amesema kua mashirikiano hayo kwa kiasi kikubwa yataweza kusaidia kutatu matatizo mbalimbali yanayoikumba sekta ya ardhi.

Nae Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kupitia sekta ya ujenzi kutoka SMT.LUDOVICK NDUHIYE amefahamisha kua kupitia mkutano huo utawezesha kurahisisha gharama za ujenzi kua nafuu pamoja kuwafanya wataalamu wa taasisi  hizo kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Nao baadhi ya washiriki wa kikao hicho wamezipongeza Serikali zote mbili kwa kuandaa mkutano huo  na wameahidi kwenda kuyatekeleza kwa vitendo ili kuweza kuleta tija kwa Serikali na jamii kwa ujumla.

Mkutano huo uliambatana na utiaji saini wa hati za makubaliano baina ya pande mbili hizo.