Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi na Kamati ya Mawasiliano Ardhi na Nishati ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakiendelea na ziara Mkoa wa Pwani pamoja na mwenyeji wao Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makaazi

katika muendelezo wa utekelezaji wa muongozo wa Ofisi ya Makamo wa Rais SMT na Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais SMZ unaoelekeza pande zote za muungano kukutana kwa lengo la kubadiishana uzoefu wa utendaji wa majukumu na namna ya kukabiliana na changamoto mbali mbali katika utekelezaji wa majukumu na kukuza ushirikiano katika usimamizi wa sekta ya Ardhi na Makaazi.

Ziara iliyofanyika tarehe 19 Oktoba 2023, Ilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Mh. Juma Makungu Juma, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Dr. Mngereza Mzee Miraji pamoja na watendaji wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi

Kwa upande wa Kamati ya Mawasiliano Ardhi na Nishati ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar iliongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Ndg. Yahya Rashid Abdallah pamoja na wajumbe wake na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makaazi iliongozwa na Mkurugenzi msaidizi wa upangaji miji na vijiji Ndugu. Imaculata Senje ambae aliwasilisha mradi wa Uwezeshaji, upangaji na uendelezaji jiji la biashara na uwekezaji Kwala- Mkoa wa Pwani.