Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Dkt. Mngereza Mzee Miraji akiongoza kikao cha pamoja na  wataalamu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makaazi SMT pamoja na mtaalamu Mr. Munseok Lee kutoka Kampuni ya Hojung Solution Co Ltd.

Kikao hicho kilihusisha majadiliano kuhusiana na uanzishwaji wa Kituo cha Ubunifu cha Mambo ya Kijografia Zanzibar  ( Zanzibar Geo-Innovation Centre ) na mradi wa National Spatial Data Infrastructure –NSDI. 
Katika tukio hilo muhimu, pia lilihudhuriwa na Mkurugenzi Mipango, Sera na Utafiti Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Ndg. Ilyasa Pakacha Haji pamoja na Mrajisi wa Ardhi Dkt. Nassir Hikmany kutoka Kamisheni ya Ardhi,   kikao kilicho fanyika tarehe 18/09/2023 Ukumbi wa Wizara Maisara Zanzibar.