Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Maakazi Dkt Mngereza Mzee Miraji akiongoza kikao baina ya Taasisi ya Kitaifa ya Kijiografia na Misitu (IGN FI) ya Ufaransa na watendaji wa Wizara yake juu ya kupitia ripoti ya upembuzi yakinifu ya Mradi wa Mfumo wa Usimamizi na Usajili wa Ardhi Zanzibar,kikao hicho kimefanyika June 27,2023.ofisini kwake Maisara Unguja

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Dk.Mngereza Mzee Miraji ameitaka kampuni inayoshughulika na miradi ya kigeografia(IGNI FI)kutoka ufaransa kuhakikisha inafata maagizo ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi katika suala zima la kuipima nchi nzima.

Aliyasema hayo huko ofisini kwake maisara alipokutana na ujumbe wa kampuni hiyo kwa lengo la kushirikiana katika masuala ya upimaji na upangaji wa ardhi.

Alifahamisha kuwa hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuondokana na changamoto za migogoro ya ardhi nchini.

Aidha Dk.Mngereza aliongeza kuwa miongoni mwa maagizo mengine ya Mhe Rais ni kuweza kuwa na mkakati maalum wa kupanga matumizi ya ardhi pamoja na kuhakikisha kuwa hakutokei udanganyifu wa utoaji ardhi moja kwa watu wawili tofauti.

Hata hivyo Katibu Mkuu huyo alifahamisha kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imejikita katika kuona migogoro ya ardhi inamalizika hivyo ni vyema kwa kampuni huyo kuzingatia maagizo hayo hayo.

Nao ujumbe kutoka Kampuni hiyo imeahidi kuyafanyia kazi maagizo yote na kuendelea kuifanya ardhi ya Zanzibar kuendelea kuwa na thamani.