Mhe Yahya Rashid Abdallah akitoa ushauri baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya wizara hiyo kwa kipindi cha april hadi Juni 2021 – 2022.
Wajumbe wa kamati ya mawasiliano ardhi na nishati ya Baraza la Wawakilishi chini ya Mwenyekiti wake Mhe Yahya Rashid Abdallah wametoa ushauri huo baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya wizara hiyo kwa kipindi cha april hadi Juni 2021 – 2022.
Wamesema dhamira ya serikali ni kuifanya ardhi kuwa kichocheo cha maendeleo na nyenzo muhimu katika kupambana na umaskini.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi dkt Mngereza Mzee Miraj akiwasilisha utekelezaji wa wizara hio ameieleza kamati kwamba wizara inaendelea na utaratibu wa uaandaaji wa rasimu ya sera ya mipango miji na vijiji ili kuhakikisha uwepo wa miji na vijiji bora na vya kisasa.