Ziara ya Mh. Waziri wa Ardhi na maendeleo ya Makaazi Zanzibar akikagua miradi ya ujenzi

Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Mhe. Rahma Kassim Ali na Naibu waziri Mhe. Salha Mohamed Mwinjuma wakitembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba katika eneo la Darajani kwa fundi Abdul ikiwa ni miongoni mwa miradi ya ujenzi inayosimamiwa na Shirika la nyumba Zanzibar.