Akizungumza na watendaji hao huko katika ofisi za Bodi hiyo Forodhani, Dkt Mngereza amefahamisha kua lengo ni kuona nyumba zote za ghorofa ambazo bodi inazisimamia kusajiliwa na kupatiwa hati miliki ili kuondokana na changamoto zinazoweza kujitokeza.
Aidha amewataka watendaji hao kusimamia vyema makusanyo ya fedha ambazo Taasisi hiyo inakusanya kupitia vyanzo vyake mbalimbali na kuhimiza uajibikaji kitendo ambacho kitapelekea kuipatia sifa Taasisi na wananchi kuendelea kujenga uaminifu kwao.
Kwa upande wake Mrajis wa Bodi ya Kondominio Majda Makame Othman ameushukuru uongozi wa Wizara ya Ardhi kwa namna inavyoshirikana katika kila hatua ya utekelezaji wa majukumu yao sambamba na kuiomba Wizara kufanyiwa kufanyiwa ukatunuzi wa jengo lao.