Akizungumza wakati alipokua akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi kupitia mfumo mpya wa manunuzi kimtandao Mkurugenzi Hamisuu aliwataka wafanyakazi hao kuyatumia ipasavyo mafunzo hayo ili kuweza kufikia lengo lililokusudiwa.
Alifahamisha kua mfumo huo ambao ulizinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwentekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi tarehe 25 july 2022 kwa lengo la kuhakikisha tunaondokana na kufanya manunuzi kwa njia ya kawaida na badala yake kuingia katika mfumo wa kisasa ili kuendana hali halisi ya sayansi na tecknolojia.
Akiwasilisha mada kuhusiana na namna ya kuweza kuutumia mfumo huo muwezeshaji kutoka mamlaka ya ununuzi na uondoshaji Mali za umma Hafidh Rashid Zam amesema kua mfumo huo utaondosha ubinafsi katika masuala ya manunuzi kwani tayari umeshaungwa moja kwa moja kupitia wakala serikali mtandao e government na utakua unaonesha kazi zote za manunuzi zinazofanywa katika Taasisi.