Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi imeanzishwa kwa tangazo la kisheria Nam: 137 ya mwaka 2020 na Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi kwa uwezo aliopewa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kifungu (1) toleo la 2010 na kukabidhiwa majukumu ya kusimamia na kuendeleza sekta za Ardhi, na Makaazi bora kwa jamii.
Kihistoria Wizara hii iliasisiwa tokea yalipofanyika Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964, ambapo ilianzishwa kama Idara ya Kazi za Umma (Public works); na kufanyiwa mabadiliko ya kimuundo katika vipindi mbali mbali na kuwa Wizara ya Ardhi, Ujenzi na Nyumba katika miaka ya 1975 – 1984; Wizara ya Maji, Nishati, na Madini katika mwaka 1984 – 1991; Wizara ya Maji, Ujenzi, Nishati, Ardhi na Mazingira katika mwaka 1991 – 2000; Wizara ya Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi mwaka 2000 – 2010 na Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati 2010, Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati 2018 na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi 2021.
DIRA:
Kuwa muhimili wa uhakika na wa usalama wa umiliki na matumizi ya Ardhi na Makaazi endelevu kwa maendeleo ya kiuchumi Zanzibar.
DHAMIRA:
Kuhakikisha kwamba Ardhi ya Zanzibar inatoa mchango mkubwa kwa ustawi wa Taifa kupitia mipango bora ya matumizi ya Ardhi kwa ajili ya huduma za makaazi na kiuchumi
MAJUKUMU:
- Kutunga na kisimamia utekelezaji wa sera za kisekta na sheria zinazohusiana na Ardhi, Nyumba na Makaazi
- Kufanya tafiti zinazohusiana na maendeleo ya sekta ya Ardhi na Makaazi
- Kutayarisha na kusimamia utekelezaji wa mipango ya matumizi bora ya Ardhi
- Kusimamia mipango ya upimaji na utoaji wa ramani za nchi
- Kusimamia utambuzi, usajili na umiliki wa Ardhi
- Kushajihisha uwekezaji katika ujenzi wa nyumba bora
MISINGI YA TAASISI:
Ujuzi, Uwajibikaji, Uwazi, Usawa, Ubunifu, Uadilifu na Mashirikiano