MAJUKUMU MAHSUSI YA OFISI YA WIZARA YA ARDHI NA MAENDELEO YA MAKAAZI 

Katika kufikia lengo la uratibu wa shughuli za Serikali, Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi imewekewa majukumu kama ifuatavyo:-

 • Kutayarisha, kuratibu na kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria na Miongozo inayohusu Ardhi, Makaazi, 
 • Kusimamia Rasilimali Ardhi kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii
 • Kuwezesha Kuwepo kwa uwiano wa matumizi ya ardhi kwa ajili ya Shughuli za Kiuchumi na Kijamii Zanzibar.
 • Kuratibu Mpango wa Maendeleo katika vijiji kwa ajili ya kukuza utalii.
 • Kuhakikisha upatikanaji wa Makaazi bora kwa Wananchi Mijini na vijijini.
 • Kuhifadhi na kuendeleza Mji Mkongwe wa Zanzibar kama ni Urithi wa Dunia.
 • Kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wote.
 • Kulinda na kusimamia miundombinu na vyanzo vya maji.
 • Kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya Nishati ilio Salama na endelevu kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
 • Kusimamia na kudhibiti matumizi ya Maji na Nishati.
 • Kusimamia Rasilimali Wat una uendeshaji wa kazi za kawaida za Wizara.
 • Kufanya mawasiliano na Taasisi zote zilizochini ya Wizara na Sekta nyengine ndani na nje ya Nchi.
 • Kufuatilia na Kutathmini Miradi ya Maendeleo iliochini ya Wizara.