Mkurugenzi ldara ya Utumishi na Uendeshaji kutoka Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Bi.Khamisuu Hamid Mohammed amesema mfumo wa manunuzi kwa njia ya kimtandao utawezesha Taasisi kufanyakazi kwa ufanisi na kuondokana na udanganyifu.
Mkurugenzi ldara ya Utumishi na Uendeshaji kutoka Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Bi.Khamisuu
Hamid Mohammed amesema mfumo wa manunuzi kwa njia ya kimtandao utawezesha Taasisi
kufanyakazi kwa ufanisi
Akizungumza wakati alipokua akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi kupitia mfumo mpya wa manunuzi kimtandao Mkurugenzi Hamisuu aliwataka wafanyakazi hao kuyatumia ipasavyo mafunzo hayo ili kuweza kufikia lengo lililokusudiwa.
Alifahamisha kua mfumo huo ambao ulizinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwentekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi tarehe 25 july 2022 kwa lengo la kuhakikisha tunaondokana na kufanya manunuzi kwa njia ya kawaida na badala yake kuingia katika mfumo wa kisasa ili kuendana hali halisi ya sayansi na tecknolojia.
Akiwasilisha mada kuhusiana na namna ya kuweza kuutumia mfumo huo muwezeshaji kutoka mamlaka ya ununuzi na uondoshaji Mali za umma Hafidh Rashid Zam amesema kua mfumo huo utaondosha ubinafsi katika masuala ya manunuzi kwani tayari umeshaungwa moja kwa moja kupitia wakala serikali mtandao e government na utakua unaonesha kazi zote za manunuzi zinazofanywa katika Taasisi.
Muwezeshaji kutoka mamlaka ya ununuzi na uondoshaji Mali za umma Hafidh Rashid Zam amesema
kua mfumo huo utaondosha ubinafsi katika masuala ya manunuzi
Hata hivyo amewataka watendaji hao kubadilika kiutendaji na kuweza kuutumia mfumo huo bila hofu ili kwenda sambamba na kasi ya kuleta mabadiliko nchini.
Nao baadhi ya wafanyakazi hao wameupongeza uongozi wa Wizara ya Ardhi kuwapatia mafunzo hayo na wameahidi kuyafanyia kazi kwa mustakabali mzima wa kuleta mabadiliko ya kiutendaji katika Taasisi wanazozitumikia.