Mkurugenzi Idara ya Utumishi na Uendeshaji kutoka Wizara ya ardhi na Maendeleo ya Makaazi bi Khamisuu Hamid Mohammed amesema kua utunzaji wa kumbukumbu kupitia mfumo wa kieletroniki ni jambo muhimu
18 Jun 2022

Mkurugenzi Idara ya Utumishi na Uendeshaji kutoka Wizara ya ardhi na Maendeleo ya Makaazi bi Khamisuu Hamid Mohammed amesema kua utunzaji wa kumbukumbu kupitia mfumo wa kieletroniki ni jambo muhimu Featured

 

Mkurugenzi Idara ya Utumishi na Uendeshaji kutoka Wizara ya ardhi na Maendeleo ya Makaazi bi Khamisuu Hamid Mohammed amesema kua utunzaji wa kumbukumbu kupitia mfumo wa kieletroniki unaojulikana kama ni key word system utaweza kuisaidia Serikali kuepukana na upotevu wa taarifa muhimu katika Taasisi tunazozitumikia.

Mkurugenzi Idara ya Utumishi na Uendeshaji kutoka Wizara ya ardhi na Maendeleo ya Makaazi

bi Khamisuu Hamid Mohammed amesema kua utunzaji wa kumbukumbu kupitia mfumo wa kieletroniki

unaojulikana kama ni key word system utaweza kuisaidia Serikali kuepukana na upotevu wa taarifa muhimu 

Akifungua mafunzo kwa baadhi ya watendaji na watunza kumbukumbu kutoka Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi huko Maisara Mkurugenzi Khamisuu amefahamisha kua wakati umefika sasa kwa watendaji kwenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na teknolojia hivyo mfumo huo utasaidi sana Taasisi za Serikali kuweza kufikia lengo la kuleta maendeleo nchini
.
Kulingana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia imeonekana utunzaji kumbukumbu kwa njia ya kieletroniki husaidia sana usalama wa uhifadhi wa Taarifa muhimu pamoja na kutokea kwa upotevu wa taarifa hizo alisema Mkurugenzi Khamisuu.

Alifamisha kua mfumo huo tayari umeshaweka ambapo unatakiwa utumike katika Tàasisi zetu lengo ni kuondosha upotevu wa taarifa muhimu ambao hua unajitokeza na kurudisha nyuma maendeleo pamoja na ufanisi mzuri katika kazi.

Aidha amewataka watendaji hao kuhakikisha wanayatumia vyema mafunzo hayo ili kuweza kuleta ufanisi mzuri katika sehemu za kazi pamoja na  kusimamia ipasavyo utunzaji wa siri za Serikali hasa sehemu zinazohusika na utoaji na upokeaji wa barua sa Taasisi.

Amefahamisha kua baadhi ya watendaji katika taasisi hasa sehemu za upokeaji na utoaji barua wamekua wakiiuka maadili ya kazi zao kwa kutoa siri kitendo ambacho ni kunyume na utaratibu na sheria za kiutumishi.

Niwasisitize watendaji wenzangu kuacha tabia ya utoaji wa siri za barua tunazopokea kufanya hivyo ni kinyume na maadili ya kazi zetu hivyo ni vyema tukazingatia maadili na kusimamia uajibikaji alisema Mkurugenzi Khamisuu.

Akiwasilisha mada kuhusiana na mfumo huo wa uhifadhi kumbukumbu kwa njia ya kieletroniki afisa kutoka Taasisi ya nyaraka Omar Jabir Abdillahi amesema kua kutokana na mabadiliko ya kidunia Taasisi zinahitajika kutumia mfumo huo ili kuendana na mabadiliko hayo kwa lengo la kuleta ufanisi mzuri na kuepusha upotevu wa Taarifa muhimu za Serikali.

Afisa kutoka Taasisi ya nyaraka ndg. Omar Jabir Abdillahi amesema kua kutokana na mabadiliko ya kidunia Taasisi

zinahitajika kutumia mfumo huo ili kuendana na mabadiliko hayo kwa lengo la kuleta ufanisi mzuri na kuepusha

upotevu wa Taarifa muhimu za Serikali.

Kwa upande wake afisa kutoka Taasisi ya Nyaraka bi.Hafsa Haji Abeid amewaomba watendaji kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri na salama sehemu za uhifadhi kumbukumbu kwani sehemu hizo ni muhimu kwa uhifadhi wa nyaraka za Serikali.