Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ndg Joseph John Kilangi akiwanasihi wafanyakazi kupima afya zao mara kwa mara
18 Jun 2022

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ndg Joseph John Kilangi akiwanasihi wafanyakazi kupima afya zao mara kwa mara Featured

 Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Ndg.Joseph John Kilangi masisitiza haja kwa wafanyakazi na jamii kuwa na tabia ya kupima afya zao mara kwa mara kwa lengo la kuweza kujitambua nakuchukua tahadhari mapema.

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Ndg.Joseph John Kilangi masisitiza haja kwa wafanyakazi

na jamii kuwa na tabia ya kupima afya zao mara kwa mara

Akifungua mafunzo ya kujikinga na maambukizi ya ukimwi katika sehemu ya kazi kwa watendaji wa Wizara ya Ardhi huko Maisra Ndg Kilangi amesema kufanya hivyo kutasaidia kwa kiasi kikubwa uelewa wa maradhi ya ukimwi kwa wafanyakazi.

Ni vyema kwa watumishi hata jamii kua na tabia ya kupima afya zetu kwani pia tutaondoa ile hofu na uhakika wa kuweza kuishi na kujitambua kama una maambukizi ama Huna alisisitiza Ndg Kilangi.

Amefahamisha kua maradhi ya ukimwi zanzibar bado yapo na yanaathiri kwa kiasi kikubwa nguvj kazi ya taifa kwa vijana ambao ndio tegemeo la taifa la kesho pamoja na kuitaka jamii hasa wazazi kufatilia mienendo ya watoto wao ili kujiepusha na jana hilo.

Aidha alifahamisha kua maisha yanabadilika na familia zinatugemea hivyo tuchukue tahadhari katika kuona hakuna maambukizi mapya pamoja kuacha tabia ya kuwabagua wale ambayo wameathirika na maradhi hayo.

Hatutakiwi tuwatenge au kuwabagua wale ambayo tayari wameshaathirika kwani wote ni sehemu ya jamii yet tunachotiwa tukae nao na kuwapa mahitaji stahiki kama binaadamu wengine alisema Katibu Kilangi.

Akiwasilisha mada kuhusiana na hali ya ukimwi kwa sasa kwa upande wa Zanzibar Mkurugenzi Mtendaji kutoka Tume ya Ukimwi Zanzibar Ahmed Mohd Khatib amesema kua kiwango cha watu walioambukizwa na maradhi hayo kinatisha ambayo ni sawa na asilimia zero nukta nne na waathirika zaidi ni vijana,wanawake na mama wajawazito.