Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Mhe.Rahma Kassim Ali atoa agizo zito
18 Jun 2022

Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Mhe.Rahma Kassim Ali atoa agizo zito Featured

 

WAZIRI wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Mhe Rahma Kassim Ali ameagiza kusimamishwa kwa ujenzi wa nyumba inayodaiwa kumilikiwa na ndg Mohd Salum Hamad kutokana na eneo hilo kua na mgogoro wa ardhi na endapo atakiuka agizo hilo kwa mara nyengine Serikali itachukua hatua za kumbomolea.

Mhe Rahma Kassim Ali ameagiza kusimamishwa kwa ujenzi wa nyumba inayodaiwa kumilikiwa na

ndg Mohd Salum Hamad 

Agizo hilo alilitoa huko Mitondooni Shehia ya Kisauni Wilaya ya Magharibi B wakati alipofanya ziara yake kwa lengo la kuskiliza mgogoro unaikabili eneo hilo ambalo linadaiwa kua ni shamba la marehemu Seif Salim Said kwa kujitokeza baadhi ya madalali kukata viwanja na kuuza kinyume na utaratibu.