KIKAO CHA MASHIRIKIANO BAINA YA KATIBU MKUU WIZARA YA ARDHI NA MAENDELEO YA MAKAAZI NA MENEJA MKUU WA KAMPUNI YA HAINAN INTERNATION CO.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi, Dkt. Mngereza Mzee Miraji amekutana na kufanya kikao na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Hainan Internation Co, Bw. Zhou Tao kwa lengo la kuboresha mashirikiano baina ya kampuni hiyo na Wizara katika kuleta maendeleo ya Sekta ya Nyumba Zanzibar.
ZIARA YA MHE WAZIRI WA ARDHI WILAYA YA KUSINI-UNGUJA
Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Mhe.Rahma Kassim Ali, Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Mhe. Juma Makungu Juma (kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Mhe.Rajab Yussuf Mkasaba (wa pili kulia) pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Dkt. Mngereza Mzee Miraji wakimsikiliza kwa makini mwananchi anaelalamikia eneo lake la Ardhi liliopo Mtende (hayupo pichani)
UHAMASISHAJI SENSA
Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Mhe.Rahma Kassim Ali akizungumza na kuwahamasisha wananchi wa Kendwa Mkoa wa Kaskazini Unguja juu ya kushiriki zoezi zima la sensa linalotarajiwa kufanyika tarehe 23 Agosti, 2022
ZIARA YA KATIBU MKUU BODI YA KONDOMINIO
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Dkt. Mngereza Mzee Miraji akizungumza na watendaji wa Bodi ya Kondominio mara baada ya kufanya ziara yake huko ofisini kwao Forodhani
MAFUNZO YA MFUMO WA MANUNUZI KIMTANDAO
Mkurugenzi Utumishi na Uendeshaji Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Bi. Khamisuu Hamid Mohd Akizungumza wakati alipokua akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi kupitia mfumo mpya wa manunuzi kimtandao
MAFUNZO YA MFUMO WA MANUNUZI KIMTANDAO
Wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi wakipata mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kutumia mfumo mpya wa manunuzi kimtandao(e-procurement)
WAZIRI WA ARDHI NA MAENDELEO YA MAKAAZI
Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Mhe.Riziki Pembe Juma akisalimiana na viongozi wa Serikali waliofika katika hafla ya uzinduzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa wakadiriaji wa majenzi Tanzania uliofanyoka katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini
MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR MHE. HEMED SULEIMAN ABDULA AKIFUNGUA TAMASHA LA WIZARA YA ARDHI
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na watendaji wa Serikali pamoja wananchi waliohudhuria katika maonesho yalioandaliwa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi yaliofanyika katika viwanja vya Verde ambapo Mhe. Hemed alimuwakilisha Rais Dk. Mwinyi
WAZIRI WA ARADHI NA MAENDELEO YA MAKAAZI MHE.RIZIKI PEMBE JUMA
Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Mhe.Riziki Pembe Juma akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa wakadiriaji wa majenzi Tanzania(TIQS) uliofanyika katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini nje kidogo ya jiji la Zanzibar
MHE. RIZIKI PEMBE JUMA AKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI
Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi kwa kushirikiana na Kampuni ya” MAP’’ambayo ni Kampuni ya Wadau wa Maendeleo ya Makaazi imeandaa maonyesho ya nyumba na Makaazi yanayojulikana kwa jina la “HOME EXPO ZANZIBAR’’.
MHE. RIZIKI PEMBE JUMA AKIENDELEA NA ZIARA ZA MIGOGORO YA ARDHI HUKO KASKAZINI
WIZARA ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi imezitaka Taasisi zinazohusika na utoaji wa vibali vya ujenzi kuacha tabia ya kukaa ofisini na badala yake kushuka kwa wananchi ili kuweza kuhakikisha eneo linalopewa kibali kuwa umiliki wake ni halali.
Mhe. Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi
Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Mhe. Riziki Pembe Juma akiwa amekaa na wananchi kusikiliza malalamiko yao ya Ardhi
MHE, RIZIKI PEMBE JUMA AMEKAA KIKAO NA KAMPUNI YA PROPARTIVE INTERNATIONAL INAYOENDESHA KAZI ZA UJENZI NDANI NA NJE YA NCHI
MHE.RIZIKI PEMBE JUMA AFANYA ZIARA YA KUZITEMBELEA NYUMBA ZA VIONGOZI WA SERIKALI ZILIOPO MAZIZINI NA KILIMANI
Mkurugenzi Mkurugenzi Idara ya Utumishi na Uendeshaji wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Bi.khamisuu Hamid Mohammed akiwasikiliza KWA makini uongozi wa NMB Bank
GHAFLA FUPI YA MKONO WA KWA KHERI ALIEKUWA KATIBU MKUU WA WIZARA YA ARDHI NDG. ALI KHALIL MIRZA
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Ndg. Joseph J Kilangi akizungumza katika ghafla ya kumuaga aliekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Ndg. Ali Khalil Mirza
MHE, RIZIKI PEMBE JUMA AMEKAA KIKAO NA KAMPUNI YA PROPARTIVE INTERNATIONAL INAYOENDESHA KAZI ZA UJENZI NDANI NA NJE YA NCHI
WAZIRI WA ARDHI NA MAENDELEO YA MAKAAZI MHE. RIZIKI PEMBE JUMA
Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Mhe. Riziki Pembe Juma akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani-Zanzibar
WIZARA YA ARDHI NA MAENDELEO YA MAKAAZI
Vipaumbele vya Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022
KATIBU MKUU WA WIZARA YA ARDHI NA MAENDELEO YA MAKAAZI
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi akutana na Wanasheria wa Wizara na kuwasisitiza kufanya kazi kwa mashirikiano

ijue Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi

Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi i ilianzishwa mwaka 2018 kutokana na mabadiliko yaliofanywa na Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa uwezo alio pewa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kifungu namba 42(1) toleo la 2010 na kukabidhiwa  majukumu ya kusimamia na kuendeleza Sekta za Ardhi na Maendeleo ya Makaazi kwa maendeleo ya Wananchi wa Zanzibar.