NDG. BAKARI ALI BAKARI
Afisa Mdhamin Pemba
Utangulizi
Afisi Kuu ya Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi – Pemba ni kiungo kati ya Taasisi za Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi kwa upande Pemba ikiwa na jukumu kuu la kuratibu na kusimamia kazi zote za Wizara kwa upande wa Pemba, Afisi hii inaongozwa/kusimamiwa na Afisa Mdhamini.
Afisi hii huratibu na kusimamia masuala yote yanayohusiana na Ardhi na Makazi katika Kisiwa cha Pemba. Afisi hii ni sehemu ya muundo wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi, ikitekeleza Majukumu yake kwa kuhakikisha kuwa matumizi ya Ardhi, upangaji wa Miji, na uendelezaji wa Makaazi unafanyika kwa kuzingatia Sheria, Mipango, na Malengo ya Serikali.
Afisi hii hutumika kama kituo kikuu cha utoaji huduma za Ardhi kwa Wananchi wa Pemba, ikiwemo upimaji wa Ardhi, usajili na utoaji hati, utatuzi wa migogoro ya Ardhi, uratibu wa maendeleo ya Makazi, na usimamizi wa mipango Miji. Kupitia afisi hii, Wananchi wa Pemba hupata huduma kwa ukaribu zaidi bila kulazimika kufuata huduma hizo Unguja.
Majukumu ya Afisi Kuu Pemba
- Kuratibu, kusimamia na Kutekeleza shughuli, Mipango na utawala zinazofanywa na WAMM kwa upande wa Pemba
- Kuratibu na kuwasilisha ripoti au taarifa za utekelezaji za kila robo, nusu na mwaka kwa Katibu Mkuu wa WAMM.
- Kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi kwa upande wa Pemba
KWA MAWASILIANO ZAIDI FIKA OFISINI GOMBANI CHAKE CHAKE -PEMBA AU WASILIANA NASI:
S.L.P 128
NUKUSHI: 024 2452287
Simu: 024 2452287
BARUA PEPE: infowamm.pemba@ardhismz.go.tz
270 Barabara ya Chake -Wete, 74206 WARA -KUSNI–PEMBA, ZANZIBAR