
NDG. KHAMISUU HAMAD MOHAMMED
Mkurugenzi Utumishi na Uendeshaji
Utangulizi
Idara ya Utumishi na Uendeshaji ndio kiungo muhimu cha Taasisi zote zilizomo ndani ya Wizara ya Ardhi na Mendeleo ya Makaazi. Idara hii ina dhamana ya kusimamia masuala yote ya kiutawala na kiutumishi katika Wizara na ina jukumu la kusimamia rasilimali watu. Idara hii ina wajibu wa kuwaendeleza watendaji kielimu ili kuhakikisha ufanisi unapatikana katika uendelezaji wa kazi za kila siku za Wizara. Idara hii inasimamiwa na Mkurugenzi ambae huteuliwa na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Kazi za Idara
- Kutoa huduma za uongozi wa Rasilimali Watu na Utawala kwa wizara husika.
- Kusimamia majukumu ya vitengo vilivyo chini ya Idara.
- Kusimamia masuala ya ajira, mafunzo, kupandishwa vyeo kwa wafanyakazi wa Wizara.
- Kuratibu masuala Mtambuka yakiwemo (Ukimwi, Jinsia, Mabadiliko ya Hali ya nchi, mambo ya idadi ya watu).
- Kuhakikisha kuwepo kwa watendaji wa kutosha na wenye sifa na kuweka kumbukumbu za masuala mbalimbali yahusuyo watendaji.
- Kufanya tathmini ya utendaji wa kila mtumishi wa Wizara na kuandaa ripoti ya hali ya utumishi kila baada ya muda kwa mujibu matakwa ya sheria au maagizo maalum.
- Kufanya tathmini ya utendaji wa kila mtumishi wa Wizara na kuandaa ripoti ya hali ya utumishi kila baada ya muda kwa mujibu matakwa ya sheria au maagizo maalum.
- Kutoa huduma za kitaalamu na huduma za manunuzi na uhifadhi wa vifaa kwa ajili ya Idara nyengine.
- Kutoa huduma za uhasibu ikiwa ni pamoja na uwekaji wa kumbukumbu za hesabu, mapato na matumizi, ulipaji wa mishahara na matayarisho ya mafao ya uzeeni.
- Kuandaa na kusimamia mpango kazi wa Idara.
- Kuandaa na kusimamia bajeti ya Idara.
- Kufanya kazi nyenginezo kama zitakavyoelekezwa na Uongozi wa Wizara kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za kazi.
Vitengo vya Idara
Idara ya Utumishi ni kitengo muhimu ndani ya Wizara ya Ardhi kinachowajibika kusimamia rasilimali watu kwa kuhakikisha upatikanaji, maendeleo na ustawi wa watumishi. Idara ya Utumishi na Uendeshaji imegawanywa katika vitengo vidogo vinavyotekeleza kazi maalumu zinazohusiana na usimamizi wa watumishi. Vitengo hivi hufanya kazi kwa ushirikiano ili kuimarisha mifumo ya utendaji, kuongeza tija, na kuhakikisha utekelezaji sahihi wa sera na taratibu za utumishi wa umma.
Kitengo cha Uendeshaji: Kitengo hiki kinaongozwa na Ofisa Utawala Mkuu na kina Majukumu yafuatayo:-
- Kuweka kumbukumbu za matukio muhimu katika sehemu ya kazi
- Kusaidi kusimamia nidhamu ya wafanyakazi.
- Kuainisha maatatizo ya wafanyakazi.
- Kusimamia matumizi na matunzo ya vifaa vya wizara ikiwemo vyombo vya usafiri, magari, mitambo, samani, vifaa vya kuandikia na vifaa vya mawasiliano.
- Kusimamia majengo na mali nyengine zisizohamishika.
- Kusimamia shughuli za kiufundi na uendeshaji wa maghala ya Wizara.
- Kufanya kazi zote atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.
Kitengo cha Utumishi: Kitengo hiki kinaongozwa na Ofisa Mkuu Utumishi kikiwa na Majukumu yafuatayo:-
- Kutunza kumbukumbu sahihi za watumishi wote kulingana na rnahali alipo.
- Kukusanya takwimu na kumbukumbu zote zinazohusu mipango ya watumishi.
- Kusaidia kukadiria idadi ya watumishi wanohitaji mafunzo.
- Kufanya kazi zote atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.
Kitengo cha Kumbukumbu: Kitengo hiki kinaongozwa na Ofisa Kumbukumbu Mkuu na kina Majukumu yafuatayo:-
- Kutafuta kumbukurnbu/nvaraka/rnafaili yanayohitajiwa na wasomaji.
- Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa kurnbukumbu/nvaraka.
- Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukurnbu/nvaraka katika makundi
kulingana na somo husika (classification and boxing) kwa ajili ya matumizi ya ofisi. - Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki (file racks/cabinets) katika masjala/vyurnba vya kuhifadhia kumbukumbu.
- Kuweka kumbukumbu (barua, nyaraka nk.) katika mafaili.
- Kushughulikia maombi ya kumbukumbu /nyaraka kutoka Taasisi za Serikali.
- Kufanya kazi nyengine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.
Muundo wa Idara
