SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

WIZARA YA ARDHI NA MAEDELEO YA MAKAAZI

WAZIRI WA ARDHI NA MAENDELEO YA MAKAAZI MHE RAHMA KASSIM ALI AMEWATAKA WATENDAJI WA MAHAKAMA YA ARDHI ZANZIBAR KUZIDISHA UMAKINI KATIKA UTOAJI WA MAAMUZI YA KESI ZA ARDHI AMBAZO HUWASILISHWA MAHAKAMANI HAPO.

AKIZUNGUMZA KATIKA MUENDELEZO WA ZIARA ZAKE ZA KUTEMBELEA TAASISI ZILIZO CHINI YA WIZARA HIYO NA KUZUNGUMZA NA WATENDAJI HUKO KATIKA OFISI ZA MAHAMAKA YA ARDHHI MWANAKWEREKWE MHE RAHMA AMESEMA TAASISI HIYO INA JUKUMU KUBWA LA KUHAKIKISHA UTAOAJI WA MAAMUZI YA KESI UNAZINGATIA UMAKINI ZAIDI.

KWA UPANDE WAKE NAIBU WAZIRI WA WIZARA HIYO MHE. SALHA MOHAMMED MWINJUMA AMESISITIZA HAJA KWA WATENDAJI KUA WAADILIFU KATIKA UTENDAJI WA KAZI ZAO NA KUJIEPUSHA NA TAMAA ILI KUWEZA KUTENDA HAKI KATIKA KAZI ZA USULUHISHI WA KESI ZA MIGOGORO YA ARDHI AMBAZO HUWALISHWA MAHAKAMANI HAPO.

MAPEMA KATIBU MKUU WIZARA YA ARDHI NA MAENDELEO YA MAKAAZI KHADIJA KHAMIS RAJAB KWA SASA WIZARA TAYARI IMESHAFANYA MCHAKATO KUTOKA MAHAKAMA YA ARDHI NA KUJA MABARA YA ARDHI AMBAPO SHERIA IPO KWA MWANASHERIA MKUU KWA UTEKELEZAJI WAKE HATUA ITAKAWEZESHA TAASISI HIYO KUFANYA KAZI KWA UFANISI ZAIDI.