Aliyasema hayo katika ofisi za Taasisi hiyo Michenzani Mall katika kikao maalum kilichowashirikisha watendaji hao chenye lengo la kukuza ufanisi wa kiutendaji wa ofisi hiyo.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Mhe Salha Mohammed Mwinjuma amesisitiza haja kwa watendaji hao kua na utaratibu wa kufanya ziara za kutembelea maeneo ambayo yanafanyiwa uthamini na ili kuweza kujirizisha mara baada ya kupokea ripotia za uthamini wa eneo husika
Mapema Mthamini Mkuu wa Serikali Tahir Mussa omar amefahamisha kuwa kwa Sasa Taasisi hiyo imefanikiwa kutayarisha muongozo wa Mali na malipo ya fidia kwa wafanyakazi ambao kwa sasa umeshaanza kufanyakazi.