Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi, Mh Rahma Kassim Ali, amesema Miradi mingi inayoanzishwa na Taasisi mbali mbali za Serikali ni utekelezaji wa maagizo yanayotolewa na Serikali kuu.

Akiweka jiwe la msingi kituo cha kuuzia Mafuta cha Kikosi cha Valantia Makao Makuu ya Mtoni, amesema ujenzi huo ni kielelezo cha Utekelezaji wa majukumu ya msingi kwa kikosi cha Valantia ya kuweka mazingira bora ya Kiuchumi na Maslahi kwa Maafisa na Mskari wake.

Akitoa taarifa ya kitaalamu, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Issa Mahfoudh Haji, amesema jumla ya shilingi Bilioni moja, Milioni mia moja na Tisini na tano zimegharimu Ujenzi huo, ambao utaimarisha ongezeko la mapato na kuchangia Mfuko Mkuu wa Serikali